Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto aliyetumikishwa vitani ni muhanga si muuaji: Shuhuda

Mtoto aliyetumikishwa vitani ni muhanga si muuaji: Shuhuda

Utumikishwaji wa watoto vitani ni mada inayojadiliwa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kupitia ushuhuda wa Junior Nzita Nsuami, Balozi Mwema wa Umoja wa Matafa kuhusu utumikishwaji wa watoto vitani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Junior ambaye mwenyewe ametumikishwa vitani kwa zaidi ya miaka 10 akiwa mtoto nchini DRC na sasa ana umri wa miaka 32, amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kuhakikisha utekelezaji wa maazimio yanayopitishwa kulinda watoto hao, akizingatia kwamba wale ni wahanga na siyo wauaji.

Amemulika jinsi watoto wanavyoathirika...

(Sauti ya Junior)

Pia amepongeza juhudi za serikali ya DRC katika kutekeleza mpango kazi wa kupambana na utumikishwaji wa watoto vitani.

Amesema changamoto kubwa inayosalia ni kudhibiti kampuni binafsi za kimataifa zinazochochea mizozo nchini DRC kwa ajili ya kuchimba madini na kusababisha watoto wengine wengi kutumikishwa vitani.