Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa kijinsia huokoa maisha majanga yanapozuka: UNISDR

Usawa wa kijinsia huokoa maisha majanga yanapozuka: UNISDR

Wakati majanga ya asili yanapozuka ,ukosefu wa usawa wa kijinsia unamaanisha tofauti kati ya uhai na kifo. Hayo yamesemwa na Robert Glasser, mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR.

Glasser ni mmoja kati ya wakuu zaidi ya 100 wa mashirika ya Umoja wa mataifa , na mashirika ya kimataifa ambao wameweka saini kuchagiza kampeni ya kimataifa mjini Geneva ya mabingwa wa mradi wa usawa wa kijinsia.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa mataifa Bwana Glasser anaeleza ni kwa nini suala la usawa wa kijinsia ni muhimu sana katika ofisi yake na kwingineko

(SAUTI YA GLASSER)

“Kwanza kabisa nimeona faida hasa za ubora wa maamuzi yanayochukuliwa ukiwa sio tu na wanaume kwenye chumba cha maamuzi bali unapokuwa na wanaume na wanawake wanapojadili kuchangia maamuzi. Na nimeona mfano ndani ya shirika ubora wa maamuzi yanayochukuliwa kyzkizingatia usawa wa kijinsia ni muhimu sana”