Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi kwenye kisiwa cha Pacific cha Nauru wanapaswa kuondolewa:UNHCR

Wakimbizi kwenye kisiwa cha Pacific cha Nauru wanapaswa kuondolewa:UNHCR

Waomba hifadhi kwenye kisiwa kidogo cha kwenye bahari ya Pacific cha Nauru wanapaswa kuhamishiwa haraka kwenye mahali penye hali ya kibinadamu , umesema Umoja wa mataifa Jumanne kufuatia kufuatia kifo cha mkimbizi aliyeungua aliyeungua vibaya.

Katika wito wake shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa sana na tukio hilo la wiki iliyopita kisiwani Naurui ambako kunatumika kama kituo cha mchakato kwa wale wanaojaribu kuingia Australia.

Wafanyakazi wa UNHCR pia wanasaka taarifa kuhusu tukio linguine lililotokea leo Jumanne ambapo mwanamke wa Kisomali ameripotiwa kuungua vibaya.

Takribani wakimbizi na waomba hifadhi 2,000 wanahifadhiwa kisiwani Nauru na Manus Papua New Guinea, pia kwenye mwambao wa Australia.