Mratibu wa UM asikitishwa na vifo vya watoto kwenye mlipuko Benghazi

3 Mei 2016

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na naibu mwakilishi malumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Libya, Ali Al-Za’tari ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya watoto watatu na mwingine kujeruhiwa jumatatu mjini Benghazi.

Watoto hao wanne wameripotiwa kutoka katika familia ya Biju na wamekuwa wahanga wa vifaa vya mlipuko katika eneo la al-Hawari karibu na mji wa Benghazi.

Ali al-Za’tari ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya watoto hao , na amemtaka kila mmoja kuwa mwangalifu katika maeneo ambayo kumekuwa na mapigano , kwani hatari ya mabomu ya kutegwa ardhini ni kubwa na ipo.

Mpango wa Umoja wa mataifa Libya UNSMIL umewaonya raia kwamba maeneo waliyoshuhudia mapigano bado ni ya hatari hadi pale yatakaposafishwa na serikali, na wazazi wote wanahimizwa kuwaelimisha watoto nini cha kufanya wanaokumbana na vifaa vinavyotia mashaka.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud