Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya ugaidi vyahatarisha uhuru wa vyombo vya habari: mtalaam wa UM

Vita dhidi ya ugaidi vyahatarisha uhuru wa vyombo vya habari: mtalaam wa UM

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari, Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kujieleza kwa uwazi, David Kaye, ameonya kwamba harakati za kupambana na itikadi kali na katili huenda zikachukuliwa kama kisingigizio cha kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Bwana Kaye amesema harakati hizo zinapaswa kuwa na msingi wa kisheria na kulingana na malengo yao.

Bwana Kaye amesikitishwa kwamba baadhi ya serikali zisizo kuwa za kidemokrasia zinatumia kisingizio hicho kulenga waandishi wa habari na wanaharakati wa haki na kuwafunga kama magaidi bila kuwapeleka mbele ya sheria.

Amesema wanaoathirika si waandishi tu bali jamii nzima inayostahili kuendelea kupashwa habari kwa uhuru.