IMF yatabiri matatizo ya kiuchumi barani Afrika

3 Mei 2016

Hali ya kiuchumi inatarajiwa kuwa tete barani Afrika mwaka huu, limesema leo shirika la fedha duniani IMF, likitoa ripoti yake kuhusu uchumi wa ukanda huo. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Céline Allard, mkuu wa Idara ya utafiti ya IMF kwa ukanda wa Afrika, amesema uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 3 mwaka 2016, wakati muongo uliopita ulikua kwa takriban asilimia 6.

Sababu ya kwanza ni kupungua kwa bei za bidhaa mbali mbali hasa mafuta, changamoto hiyo ikikumba zaidi nchi zinazouza mafuta nje, kama vile Nigeria.

Hata hivyo Bi Allard amesema baadhi ya nchi bado zitashuhudia ukuaji uchumi wa zaidi ya asilimia 5, ikiwemo Kenya.

Miongoni mwa mapendekezo ya IMF ni kuimarisha ukusanyaji wa kipato cha ndani, na kuendelea kuwekeza katika miundombinu

(Sauti ya Bi Allard)

“ Kama hakuna barabara za kutosha na viwanda vya kuzalisha umeme kutakuwa vigumu kuendeleza viwanda kwa mfano. Bado tunadhani kwamba jitihada za kuimarisha miundombinu zinahitajika sana.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter