Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahusika wa ghasia dhidi ya waandishi habari Sudan Kusini waorodheshwe na kuwajibishwa:UNESCO

Wahusika wa ghasia dhidi ya waandishi habari Sudan Kusini waorodheshwe na kuwajibishwa:UNESCO

Wahusika wa ghasia dhidi ya waandishi wa habari Sudan Kusini waorodheshwe na kuwajibishwa limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Wafanyakazi saba wa vyombo vya habari walipoteza maisha mwaka 2015 wakati taifa hilo changa la afrika likishuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wafanyakazi saba wa vyombo vya habari walipoteza maisha mwaka 2015 wakati taifa hilo change la afrika likishuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Leo wakati dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani chini ya kauli mbiu “fursa ya kupata habari na uhuru wa msingi, UNESCO imekumbusha umuhimu wa kuwalinda waandishi wa habari. Sani Martin amezungumza na Lydia Gachungi kutoka kitengo cha habari na mawasiliano, UNESCO Sudan Kusini.

(SAUTI YA LYDIA GACHUNGI)

"Wakati wananchi na waandishi habari wanapewa fursa ya kupata taarifa hususan taarifa kuhusu taasisi za umma, hii ndio taarifa inayowawezesha raia kutekeleza wajibu wao katika kuendeleza demokrasia na usimamizi mzuri na uwajibikaji. Bila taarifa muhimu mtu wa kawaida hawezi kupata huduma muhimu, au kutekeleza haki yake ya kupiga kura."