Skip to main content

Mkimbizi wa Syria abeba mwenge wa olimpiki

Mkimbizi wa Syria abeba mwenge wa olimpiki

Kwa mara ya kwanza mashindano ya Olimpiki mwaka huu yatakayo fanyika nchini Brazil baadaye mwaka huu, yametoa fursa kwa wakimbizi kushiriki. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, hii ni fursa nzuri kuonyesha mshikamano na wakimbizi na wahamiaji.

Timu maalumu ya wakimbizi itashindana chini ya mwamvuli wa bendera ya Olimpiki na miongoni mwa watakaoshiriki mashindano ya mwaka huu ni mkimbizi kutoka Syria aliyepata fursa pia ya kukimbiza mwenge wa Olimpiki kwenye kambi ya wakimbizi ya Eleonas nchini Ugiriki. Ambatana na Assumpta Massoi katika makala hii kwa undani zaidi.