Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

De Mistura akutana na John Kerry ili kuokoa sitisho la mapigano Syria

De Mistura akutana na John Kerry ili kuokoa sitisho la mapigano Syria

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura amekuwa na mkutano leo na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, kwa ajili ya kurejesha sitisho la mapigano nchini humo. Sitisho hilo lilianzakutekelezwa mwezi Februari mwaka huu lakini limetatizika kwenye baadhi ya maeneo kwa kipindi cha wiki chache zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Bwana de Mistura amesema utashi wa kisiasa unahitajika ili kuimarisha sitisho hilo la mapigano.

(Sauti ya de Mistura)

“Marekani na Urusi ndio walioweza kufanya muujiza, tarehe 27 Februari. Sasa muujiza umekuwa tete sana, kiasi kwamba uko hatarini kabisa. Hakuna kisingizio cha kutotafuta tena, kuanzisha na kutekeleza upya kile kilichokuwa au ujumbe mkubwa zaidi wasyria waliosikia kutoka kwetu sote.”

Amesema kinachoendelea ni kuanzisha utaratibu mpya wa kufuatilia na kuhakikishia sitisho la mapigano.

Baada ya mazungumzo na John Kerry, Bwana de Mistura atasafiri mjini Moscow ili kuzungumza na wawakilishi wa Urusi.