Skip to main content

UNEP lakariri msimamo wake dhidi ya ujangili wa tembo.

UNEP lakariri msimamo wake dhidi ya ujangili wa tembo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira,UNEP limekariri msimamo wake wa kupambana na ujangili wa wanyamapori, wakati ambapo tani 105 za pembe za ndovu na vifaru zimeteketezwa kwa moto na serikali nchini Kenya mwishoni mwa wiki. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte .

(Taarifa ya Priscilla)

Akihudhuria hafla hiyo Naibu Mkuu wa UNEP Ibrahim Thiaw amesema kuchoma pembe hizo kumetuma ujumbe mkali kwa jamii ya kimataifa kwamba ujangili hauwezi tena kukubaliwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP Helen Clark amesema jitihada za Umoja wa Mataifa zinapaswa kuongeza kasi, akieeleza

(Sauti ya Bi Clark)

“Kutunza wanyamapori ni sehemu ya maendeleo endelevu ya Kenya. Kweli jangili atapata kiasi cha pesa kupitia tembo aliyeuawa. Lakini tembo huyu akiwa hai ana thamani zaidi kuliko akiuawa.”

Rais wa Kenya, Uganda na Gabon walihudhuria pia tukio hilo.

Kwa mujibu wa UNEP, zaidi ya ndovu 100,000 wameuawa tangu 2010 na wanyama hao wako hatarini kutoweka kabisa iwapo ujangili hautakomeshwa.