Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Katibu Mkuu ahitimisha ziara ya masuala ya kibinadamu Nepal

Naibu Katibu Mkuu ahitimisha ziara ya masuala ya kibinadamu Nepal

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Jan Eliasson amehitimisha ziara yake ya masuala ya kibinadamu nchini Nepal hii leo Jumatatu. Amina Hassan na taarifa kamili

(TAARIFA YA AMINA)

 Katika siku tatu za ziara hiyo Bwana Eliasson amekutana na waziri mkuu Oli na Rais  Bidhya Devi Bhandari pamoja na maafisa wengine wa serikali.

Azima kuu ya ziara hiyo imekuwa ni kukutana na kuzungumza na jamii iliyoathirika na tetemeko la ardhi la mwaka 2015 , kama sehemu ya “mpango maalumu wa masuala ya kibinadamu” katika kuelekea mkutano mkuu wa kimataifa wa masuala ya kibinadamu utakaofanyika Istanbul Uturuki kuanzia Mai 23-24 mwaka huu. Miongoni mwa maeneo aliyotembelea ni jamii ya wakulima ya Irkuk na kituo maalumu kwa ajili ya wanawake Chautara Alipokutana na waathirika wa tetemeko hilo Eliasona akasema

(SAUTI YA JAN ELIASSON)

"Pamoja ndio neno muhimu kwenye dunia ya leo. Hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu, lakini kila mtu anaweza kufanya kitu kimoja. Na nasena, kila mtu anapaswa kufanya kitu kimoja ili kuonyesha msshikamano. Maumivu ya watu wenu ni maumivu ya dunia nzima."

Bwana Eliasson anaendelea na mpango huo wa masuala ya kibinadamu ambapo baada ya kuondoka Nepal anakwenda Vietnam.