Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa malaria na juhudi za kuutokomeza Tanzania

Ugonjwa wa malaria na juhudi za kuutokomeza Tanzania

Tarehe 25 mwezi Aprili ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya malaria, msisistizo ukiwa kutokomeza ugonjwa huo. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguniWHO, takribani watu bilioni 3.2 ambayo ni karibu nusu ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kuambikizwa malaria.

Mwaka 2015 visa zaidi ya milioni 200 vya malaria viliripotiwa na zaidi ya vifo Laki Nne. Bara la Afrika hususani nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinabeba mzigo mkubwa ambapo WHO inasema kwamba mwaka 2015 bara hilo lilikuwa na asilimia 89 ya visa vya malaria na asilimia 91 ya vifo.

Katika kuadhimisha siku ya malaria duniani mwaka huu, WHO imesema lengo la kutokomeza ugonjwa huo katika nchi 35 ifikapo mwaka 2030 linaweza kufanikiwa licha ya kuwa ni la juu.

Ikitolea mfano wa bara Ulaya ambalo kwa mwaka 2015 halikuwa na kisa chochote, WHO imesema kunahitaji uwekezaji mkubwa na wa dharura kutokomeza ugonjwa huo huku akipongeza nchi za Afrika zilizo kwenye mwelekeo sahihi.

Tuelekee Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania, kutazama hali ya malaria na juhudi za kuutokomeza ugonjwa huo. Mwenyeji wetu ni Martin Nyoni wa redio washirika redio SAUTI ya Mwanza Tanzania.