Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wajiandaa kwa kongamano Korea Kusini: Elimu Kwa Uraia wa Ulimwengu

Vijana wajiandaa kwa kongamano Korea Kusini: Elimu Kwa Uraia wa Ulimwengu

Kongamano la 66 la Idara ya Habari ya Umoja wa Mataifa na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) litafanyika mjini Gyeongju, Korea Kusini, kuanzia Mei 30 hadi Juni mosi, 2016, na tayari maandalizi yameanza.

Kauli mbiu ya kongamano hilo ni Elimu kwa Uraia wa Ulimwengu: Kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu Pamoja.

Wakati huu, asasi za kiraia zinazohusika na maendeleo ya vijana zinaandaa ajenda ya kuchukua hatua, ambayo itajumuisha maoni ya vijana na mapendekezo kuhusu elimu kwa uraia wa ulimwengu na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Ni katika muktadha huo, ndipo mkutano umefanyika jijini New York hapo jana, ukiwaleta vijana pamoja kubadilishana mawazo kuhusu ajenda ya kongamano la Korea Kusini. Je ni nini kilichojiri? Ungana na Flora Nducha katika makala hii