Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kisumu Kenya mstari wa mbele katika jaribio la mkakati wa Sendai

Kisumu Kenya mstari wa mbele katika jaribio la mkakati wa Sendai

Mji wa Kenya wa Kisumu unaongoza mashiniani katika kutekeleza makubaliano ya Sendai ya kupunguza majanga barani Afrika katika juhudi za kutafuta suluhu endelevu kukabiliana na changamoto ya ukauji wa miji na mabadiliko ya tabianchi.

Hii ni kufuatia kumalizika kwa jaribio la kwanza ambalo litasaidia serikali ya mitaa kupima mafanikio ya mkakati wa Sendai, ambayo yaliafikiwa na jamii ya kimataifa Machi mwaka 2015, kwa ajili ya kupunguza athari za majanga yanayozuilika na yasiyozuilika.

Kisumu ambao ni mjii mkuu wa tatu nchini Kenya ulitoa kipaumbele kwa maswala ya kupunguza majanga kwa kujiunga na kampeni ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji hatari ya majanga, UNISDR, ambayo kwa sasa ina wanachama 3,000.

Kampeni hiyo imetaja majaribio kumi muhimu ya kutafiti uhimili wa miji ambayo Kisumu inatarajia kutekeleza.