Ukame na kuanguka kwa bei ya mafuta kwaongeza mahitaji ya kibinadamu Angola

29 Aprili 2016

Watu milioni 1.4 katika mikoa 18 nchini Angola wameathiriwa na ukame mkubwa uliosababishwa na hali ya hewa ya El Niño nchini humo, wakihitaji usaidizi wa kibinadamu, kwa mujibu wa ofisi ya Mratibu Mkaazi wa Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu nchini humo (OCHA).

Asilimia 80 ya watu walioathirika wanaishi katika mikoa ya kusini mwa nchi ya Cunene, Huila na Namibe.

Viwango vya unyafuzi vimeongezeka maradufu, ikilinganishwa na takwimu za nusu ya kwanza ya 2015, ambapo watoto 95,000 wameathiriwa, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF.

Kwa mujibu wa OCHA, uhakika wa kuwa na chakula unatarajiwa kuwa mbaya zaidi kuanzia Julai hadi mwishoni mwa mwaka 2016 kwa sababu ya mavuno kidogo na mafuriko yaliyoletwa na La Niña.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter