Mauaji ya Burundi ni dhihirisho la machafuko yanayoenea- Zeid

Mauaji ya Burundi ni dhihirisho la machafuko yanayoenea- Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein, amelaani idadi inayoongezeka ya mashambulizi dhidi ya maafisa waandamizi wa serikali nchini Burundi, kufuatia mauaji ya Brigedia-Jenerali Athanase Kararuza na mkewe, na jaribio la kumuua waziri siku moja kabla.

Katika taarifa, Kamishna Zeid amesema mashambulizi hayo ya hivi karibuni ni dhihirisho la kuenea kwa ghasia za kikatili nchini Burundi, na kwamba huenda yakachochea ghasia zaidi.

Angalau watu 31 wameuawa mwezi Aprili mwaka 2016 pekee, ikilinganishwa na idadi ya watu tisa waliouawa mwezi Machi.

Ravina Shamdasani, ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu, Geneva:

“Kamishna Mkuu amelaani vikali mashambulizi haya. Ni lazima yachunguzwe ipasavyo, na waliotenda mauaji ni lazima wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria. Mengi ya mashambulizi haya yalifanywa na wanaume wenye silaha wasiojulikana.”