Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kulinda amani Côte d'Ivoire kufungwa karibuni:

Mpango wa kulinda amani Côte d'Ivoire kufungwa karibuni:

Jukumu la mpango wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Côte d'Ivoire UNOCI utaongezwa muda kwa muhula wa mwisho limeamua baraza la usalama la Umoja wa mataifa.

Wajumbe 15 wa baraza la usalama wamepitisha azimio Alhamisi ambalo linaongeza muda wa mwisho wa UNOCI hadi mwisho wa mwezi Juni mwaka 2017. Na mara utakapofungwa jukumu lake litachukuliwa na serikali ya Côte d'Ivoire na timu ya Umoja wa mataifa nchini humo.

Mpango wa UNOCI ulianzishwa mwaka 2004 ili kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya amani kufuatia kumalizika kwa miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.