Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yakutanisha vijana wa Afrika kuhusu urithi wa dunia

UNESCO yakutanisha vijana wa Afrika kuhusu urithi wa dunia

Vijana kutoka kanda ya Afrika wanakutana kwenye kisiwa cha Robben huko Afrika Kusini, katika kongamano la Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuhusu urithi wa dunia. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Kongamano hilo linaloanza leo Aprili 28 hadi tarehe 4 Mei 2016, ni sehemu ya programu ya UNESCO ya elimu kuhusu urithi wa dunia, na linalenga kutoa jukwaa la kuongeza ushiriki wa vijana katika kuendeleza na kutunza urithi wa dunia barani Afrika.

Kongamano hilo pia linalenga kuongeza uelewa wa UNESCO na wadau wake kuhusu changamoto wanazokumbana nazo vijana, mafanikio yao, na hatua zinazohitajika katika kutekeleza mkataba wa urithi wa dunia barani Afrika.