Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa wanawake ni muhimu sana katika kuleta amani:Gambari

Mchango wa wanawake ni muhimu sana katika kuleta amani:Gambari

Mjadala kuhusu mchango wa wanawake katika ujenzi wa amani hususani kwenye maeneo yanayokumbwa na vita ni lazima uendelee licha ya kuwepo kwa azimio a Umoja wa mataifa kuhusu suala hilo lililopitishwa mwaka 2000.

Hayo yamesemwa na Bwana Ibrahim Gambari mwakilishi maalumu wa zamani wa Umoja wa mataifa na mkuu wa UNAMID, na ambaye kwa sasa ni Rais wa kituo cha Savannah kwa ajili ya diplomasia na maendeleo mjini Abuja Nigeria alipozungumza na Radio ya Umoja wa mataifa.

Amesema dunia imebadilika, vita viomeongezeka, ugaidi, na hata ukatili dhidi ya wanawake, hivyo umefika wakati wa kutekeleza azimio kwa vitendo

(SAUTI YA GAMBARI)

Changamoto imeongezeka hivyo kunahitajika juhudi zaidi zinazoendelea kwa upande wa kila mtu, serikali, asasi za kiraia na mashirika yaliyojikita katika masuala haya , kuja pamoja ili kutafsiri na kilifanya azimio hilo kuwa hali halisi”