Skip to main content

Mwaka mmoja baada ya tetemeko Nepal yaanza ujenzi mpya

Mwaka mmoja baada ya tetemeko Nepal yaanza ujenzi mpya

Moja ya miradi mashuhuri duniani ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kuwahi kuendeshwa unaanza wiki hii kufuatia kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuzuka tetemeko la ardhi nchini Nepal mwexi April mwaka jana.

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti hatari ya majanga UNISDR, mamlaka ya ujenzi ya Nepal na washirika wake wanaanza mpango huo ili kutoa nyumba zaidi ya 500,000 za gharama nafuu na zinazohimili tetemeko la ardhi kwa watu milioni tatu ambao ytayari wamekuwa katika makazi ya muda msimu mzima wa mvua na majira ya baridi.

Serikali ya Nepal imesema kutokana na upungufu wa mafundi ujenzi walio na elimu ya kutosha na vifaa vingine, ujenzi huo utachukua hadi miaka mine kukamilika.

Tetemeko la mwaka jana Nepal lilikatili maisha ya watu zaidi ya 8000, maelfu wengine kujeruhiwa na watu milioni tatu walipoteza makazi yao.