Ujio wa Machar Juba na nuru ya amani Sudan Kusini
Nchini Sudan Kusini nuru ya amani imeanza kuchomoza, kufuatia hatua inayolezwa kuwa ya kihistoria ya kurejea mjini Juba kwa makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar. Ungana na Joseph Msami katika makala inayokusimulia kinagaubaga matumaini yaliyogubika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, baada ya kuwasili kwa kiongozi huyo.