Baraza Kuu na lile la usalama yapitisha maazimio kuhusu ujenzi wa amani

27 Aprili 2016

Maazimio kuhusu ujenzi wa amani kwenye mizozo yamepitishwa leo kwa kauli moja na baraza la usalama na baraza kuu, maazimio yaliyoelezwa kulenga kutatua changamoto zinazokabili amani ya kudumu. Flora Nducha na maelezo kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Azimio hilo ni matokeo ya majadiliano baina ya nchi wanachama yaliyoratibiwa ana Angola na Australia kulingana na utafiti na mapendekezo ya kundi la wataalamu washauri katika ripoti ilioitwa changamoto ya kudumisha amani.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii muda mfupi kabla ya kupitishwa kwa azimio hilo mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa ujenzi wa amani PCB, ambaye ni mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika ofisi za Umoja huo mjini New York balozi Macharia Kamau, amezungumzia umuhimu wa azimio hilo.

(SAUTI KAMAU)

Kadhalika amezungumzia nafasi ya wanawake na vijana katika ujenzi wa amani.

( SAUTI KAMAU)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter