Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM ya uchunguzi dhidi ya vitendo vya Israel kuzuru Amman na Cairo

Kamati ya UM ya uchunguzi dhidi ya vitendo vya Israel kuzuru Amman na Cairo

Kamati maalumu ya Umoja wa mataifa ya kuchunguza vitendo vya Israeli vinavyoathiri haki za binadamu za watu wa Palestina na Waarabu wengine kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa, watafanya ziara ya kila mwaka mjini Amman Jordan na Cairo Misri.

Katika ziara yao inayoanza Mei mosi hadi Mei 8, kamati hiyo itakutana na waathirika, wawakilishi wa jamii, mashahidi, mashirika yasiyo ya kiserikali ya upande wa Israeli na Palestina, maafisa wa serikali ya Misri, Jordan, Palestina na wawakilishi wa Umoja wa mataifa , ili kupata ushahidi n kusikikliza maelezo kuhusu masuala mbalimbali yanohusu haki za binadamu yanayotia hofu katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na milima ya Golan Syria.

Kamati hiyo imewasiliana na serikali ya Israeli kupata fursa ya kufikia maeneo ya Wapalestina lakini mpaka sasa haijapata majibu yoyote kutoka kwa serikali ya Israeli.

Kamati hiyo itatoa taarifa mwishoni mwa ziara yake na kisha ripoti itakayowasilishwa kwenye kikao cha 71 cha baraza kuu mwezi Septemba.