Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza mamlaka ya MINUSCA hadi Julai 31, 2016

Baraza la Usalama laongeza mamlaka ya MINUSCA hadi Julai 31, 2016

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kuongeza muda wa mamlaka ya Ujumbe wa Umoja huo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), hadi Julai 31, 2016, likisema hali nchini humo bado ni tishio kwa amani na usalama kimataifa.

Azimio hilo namba 2281(2016) pia linataoa mamlaka kwa MINUSCA kuchukua hatua zote zinazohitajika katika kutekeleza wajibu wake kulingana na uwezo wake na maeneo unapohudumu.

Halikadhalika, Baraza hilo limemwomba Katibu Mkuu kufanya tathmini ya kimkakati kuhusu MINUSCA, ili kuhakikisha kwamba mamlaka ya ujumbe huo katika siku zijazo yanabadilika sanjari na mazingira yatakayowezesha ujenzi wa amani baada ya kumalizika kipindi cha mpito na kurejeshwa utulivu, na kutoa ripoti kwa Baraza hilo mnamo Juni 22, 2016.