Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yatuma ujumbe Syria kutathimini uharibifu wa Palmyra

UNESCO yatuma ujumbe Syria kutathimini uharibifu wa Palmyra

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO limetuma ujumbe wa haraka wa kutathimini eneo la urithi wa dunia nchini Syria,  Palmyra.

Taarifa ya UNESCO inasema ujumbe huo unaopaswa kufanya kazi yake kwa siku siku mbili yaani Aprili 24 hadi 26, unapaswa kuainisha mbinu za dharura za ulinzi wa eneo hilo baada ya tathimini ya jumla ikiwamo uharibifu wa eneo na makumbusho.

Ujumbe huo pia umeelezwa kuwa utaeleza wajibu wa awali na taratibu kwa ajili ya hatua za uratibu wa jumuiya ya kimataifa.

Taarifa ya UNESCO imemnukuu Mkurugenzi Mkuu Irina Bokova akitaja kanuni za tathimini ya Palmyra ambapo amesisitiza kuwa ni kuepusha uharibifu zaidi, akitaka uratibu na hatua za pamoja na kuongeza kwamba UNESCO itaandaa mkutano wa kimataifa wa wataalamu kuhusu hatua za dharura za kulinda maeno ya kitamaduni ya Syria utakaofanyika mjini Berlin Juni mbili hadi nne.