Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kurejea kwa Riek Machar Juba kunatia matumaini- Herves Ladsous

Kurejea kwa Riek Machar Juba kunatia matumaini- Herves Ladsous

Hali nchini Sudan Kusini bado inatia wasiwasi, lakini kurejea kwa Dkt. Riek Machar Juba ni hatua inayoleta matumaini, amesema leo Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa, Herves Ladsous akilihutubia Baraza la Usalama. Taarifa ya Joshua Mmali inafafanua,

(TAARIFA YA JOSHUA)

Taarifa kamili na Joseph Msami

Bwana Ladsous amesema kufuatia kurejea kwa Dkt. Machar Juba, ni muhimu mwelekeo wa kisiasa na kiusalama nchini humo humo sasa ubadilike haraka, ili kuwezesha mchakato wa amani kufanikiwa. Tayari inaripotiwa kuwa Dkt. Machar ameshaapishwa kama Makamu wa kwanza wa rais.

Bwana Ladsous amesema, hatua hiyo inafungua ukurasa mpya nchini Sudan Kusini.

“Itawezesha mchakato halisi wa mpito kuanza. Ni muhimu pande zote kuchukua fursa hii na kuonyesha nia na dhamira ya kuendeleza mchakato wa amani. Kutakuwa na hatua mbili muhimu zitakazofuata. Mosi, ni kuunda serikali ya mpito na serikali ya muungano wa kitaifa, na pili, kutekeleza hatua za mpito za usalama”