Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Australia ilikiuka haki za viziwi kuhudumu mahakamani- wataalam wa UM

Australia ilikiuka haki za viziwi kuhudumu mahakamani- wataalam wa UM

Wataalam wa Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu  haki za watu wenye ulemavu, wamesema kuwa haki za viziwi nchini Australia zilikiukwa pale walipoitwa kuhudumu kwenye baraza la waamuzi wa mahakama lakini hawakuwezeshwa kufanya hivyo. Kwa mujibu wa wataalam hao, ingawa viziwi hao walisajiliwa kuhudumu kwenye uendeshaji kesi mahakamani, waliambiwa kwamba wasingeweza kupewa usaidizi waliohitaji wa mkalimani wa lugha ya ishara au maneno kuchapishwa moja kwa moja ili waweze kushiriki.

Damjan Tatic, ambaye ni mwanakamati hiyo, amesema nchi zilizoridhia Mkataba kuhusu haki za watu wenye ulemavu kama Australia zinahitajika kufanya maandalizi ya kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kufurahia haki sawa na watu wengine, na kushiriki kikamilifu katika nyanja zote za maisha.