Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za Batwa zinakiukwa Rwanda:Asasi za kiraia

Haki za Batwa zinakiukwa Rwanda:Asasi za kiraia

Jamii ya walio wachache nchini Rwanda ijulikanayo kama Batwa haki zao zimekuwa zikiiukwa nchini Rwanda amesema Niyomugabo Hdephonse mwakilishi wa shirika la kiraia la Yuouth Potters Development alipoozungumza kwenye kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi inayoendelea na kikao chale leo mjini Geneva Switzerland.

Amesema jamii hiyo ambayo ina watu takribani 35,000 wamepoteza makazi yao ya msituni na hawajapewa mbadala wa maisha yao. Pia amesema kutokuwa na uwakilishi wa jamii hiyo serikalini ni suala linalotoa hiofu kuhusu mustakhbali wao, wakati serikali ikiendelea kukataa kutambua uwepo wa jamii hiyo nchini Rwanda ikiendelea na sera ya kuwakandamiza.

Amesema Batwa wameendelea kubaguliwa na kuwa na uwakilishi mdogo katika ngazi ya jamii hata kitaifa, wana elimu ndogo sana na mara nyingi hawatambui haki zao na hawajui jinsi ya kuwasilisha malalamiko. Lazima kuwe na sera ya kulinda haki za Batwa.