Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM aitaka Somalia iwajibishe wanaotenda ukatili wa kingono

Mtaalam wa UM aitaka Somalia iwajibishe wanaotenda ukatili wa kingono

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga, ametoa wito kwa serikali ya Somalia iimarishe uwezo wa vyombo vya sheria na vikosi vya polisi katika kushughulikia kesi za ukatili wa kingono na kijinsia.

Bwana Nyanduga ameitaka serikali hiyo pia ipige marufuku kesi hizo kushughulikiwa na wazee wa kaya za kijadi, akisema ukatili wa kingono ni lazima ukabiliwe kisheria kama kosa la jinai.

Aidha, ametoa wito kwa serikali ya Somalia itekeleze mapendekezo yaliyotokana na tathmini ya mwaka 2016 katika Baraza la Haki za Binadamu, yakiwemo kuridhia sitisho la kutekeleza adhabu ya kifo.