Skip to main content

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais Kabila

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais Kabila

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila na kujadiliana kuhusu  hali ya usalama nchini humo na utekelezaji wa mamlaka ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu ameitaka serikali kuchukua hatua  muhimu ili kuondoa mivutano ya kisiasa na kuleta amani nakuandaa mazingira mujarabu ya  uchaguzi wa Rais na wabunge kulingana na katiba.

Ban pia ameitaka serikali ya DRC kuendelea na jitihada za majadiliano ya kimakakati na MONUSCO ikiwamo maendeleo ya mkakati wa awali kwa ajili ya MONUSCO. Katika mazungumzo baina ya Rais Kabila na Katibu Mkuu wa Umoaj wa Mataifa, suala la mkutano wa dunia wa misaada ya kibinadamu utakaofanyika nchini Urutuki limeibuka ambapo Ban amesisitiza umhimu wa mkutano huo huku pia akielezea matumaini yake kuhusu mkataba wa Paris uliosainiwa mwishoni mwa juma.

Amesema anaamini mkataba huo wa mabadiliko ta tabianchi utapitishwa hivi karibuni nchini humo. Rais Kabila ametia saini mkataba huo kwa niaba ya serikali ya DRC.