Hatuna uchaguzi katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi- Balozi Manongi

Hatuna uchaguzi katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi- Balozi Manongi

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo kwazo athari za mabadiliko ya tabianchi ziko dhahiri. Mathalani kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari na hivyo kutishia uwepo wa visiwa, halikadhalika mizozo kati ya wakulima na wafugaji katika kusaka malisho. Je nini kinafanyika na je kutiwa saini mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kunaashiria nini? Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa amezungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kabla ya kutia saini mkataba huo kwa niaba ya nchi yake. Hapa anaanza kwa kuelezea athari za mazingira Tanzania.