Mabadiliko ya tabia nchi ni changamoto kubwa katika kizazi hiki:Dicaprio

22 Aprili 2016

Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa katika kizazi hiki na wakati ni sasa wa kuchukua hatua madhubuti na za kijasiri, amesema leo mcheza filamu nyota hilimate Leonardo DiCaprio

Mjumbe huyo wa umoja wa mataifa wa amani alikuwa akihutubia wakati wa hafla maalumu ya utiaji saini wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mwanamazingira huyo ambaye pia ni sauti ya kuchagiza masuala ya hali ya hewa amewataka viongozi wa dunia kuwajibika katika kuongoza, kuhamasisha na kuwezesha akionya kwamba dunia inawaangalia na ama watashukuriwa au kulaumiwa na vizazi vijavyo

(SAUTI YA LEONARDO DICAPRIO)

"Sasa hebu fikiria kuhusu aibu ambayo kima mmoja wetu ataibeba wakati watoto na wajukuu zetu wakitafakari na kubaini kwamba tulikuwa na uwezo wa kukomesha madhila, lakini eti tukakosa tu utashi wa kisiasa kufanya hivyo. Ndio tufanikiwa mkataba wa Paris lakini kwa bahati mbaya ushahidi unatuonyesha kwamba huo pekee hautotosha.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter