Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP22 kufanyika Marrakech Morocco: Binti Mfalme Lala Hasna

COP22 kufanyika Marrakech Morocco: Binti Mfalme Lala Hasna

Morocco imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza kutia saini mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Matafa na kuahidi kuchukua hatua zote za lazima kuuridhia haraka iwezekanavyo .

Akizungumza kwenye hafla hiyo maalumu ya utiaji saini binti mfalme wa Morocco Lala Hasna ameipongeza Ufaransa kwa kuwa Rais wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris COP21 na kusema wakati hii wakijiandaa na COP22 ambao Morocco imepata heshima ya kuwa mwenyeji mjini Marrakech, juhudi za pamoja lazima zijikite kwenye utekelezaji wa mkataba huo.

(SAUTI PRINCESS LALA HASNA)

“Katika kutimiza wajibu wa mabadiliko ya tabia nchi , ufalme wa Morocco umepitisha sera ya kitaifa kuhakikisha mazingira yanalindwa , kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza gesi chafuzi kwa asilimia 32 ifikapo 2030”

Ameongeza kuwa hivyo Morocco imezindua miradi mbalimbali ya kuchagiza uchumi unaojali mazingira, umepitisha sheria ya kitaifa ya kulinda mazingira pamoja na mikakati ya mjarabu ya sekta ya nishati. COP 22 itaanza Marrakesh Novemba 7 hadi 18 mwaka 2016.