Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaonya wakimbzi wa Burundi kumiminika zaidi nchi jirani

UNHCR yaonya wakimbzi wa Burundi kumiminika zaidi nchi jirani

Mwaka mmoja tangu kuzuka kwa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema idadi ya wakimbizi wa nchi hiyo wanaosaka hifadhi nchi jirani inaongezeka na sasa imefikia 260,000. Tarifa zaiodi na Pariscilla Lecomte.

(TAARIFA YA PRSCILLA)

Taarifa ya UNHCR inasema kuwa ikiwa suluhisho la kisiasa halitapatikana maelfu zaidi ya wakimbizi wanatarajiwa ambapo pia imeelezwa kuwa wengi wa wakimbizi wanasimulia kutendewa vitendo vilivyo kinyume na haki za binadamu ikiwemo kuuwawa na mateso.

Shirika hilo limetaka usaidizi wa jumuiya ya kimataifa hususani katika majadiliano jumuishi ya kusaka suluhu.

UNHCR hata hivyo imefafanua kuwa katika siku za usoni wakati wa kurejea kwa wakimbizi nchini humo, itawekeza katika elimu kwa watoto na vijana, na kuwahamasisha wakimbizi kujitegemea kutokana na upungufu wa ufadhili wa fedha. Miongoni mwa nchi jirani zinazobeba mzigo wa wakimbizi wa Burundi ni Tanzania.