Mkataba wa Paris kuanza kutiwa saini leo New York

22 Aprili 2016

Hatimaye mkataba wa Paris kuhusu tabianchi unaanza kutiwa saini leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kuanzia leo tarehe 22 Aprili 2016.

Kuanza kutiwa saini kwa mkataba huo ni kiashiria cha nchi wanachama wa mkataba huo kuchukua hatua kuelezea nia yao ya kutekeleza yaliyomo ndani ya mkataba huo ambapo Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi ambaye atatia saini kwa niaba ya nchi yake amesema..

(Sauti ya Balozi Manongi)

Balozi Manongi akaelezea matumaini baada ya kutiwa saini mkataba wa Paris.

(Sauti ya Balozi Manongi)

Kalamu maalum imeandaliwa kwa ajili ya utiaji saini mkataba huo uliopitishwa mwezi Disemba mwaka jana huko Paris, Ufaransa na ambao utakuwa wazi kwa ajili ya kutiwa saini hadi tarehe 22 Aprili mwaka 2017.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter