Twatiwa moyo na utiwaji saini mkataba wa tabianchi- MJUMITA

Twatiwa moyo na utiwaji saini mkataba wa tabianchi- MJUMITA

Tarehe 22 Aprili mwaka 2016 ni siku ya kihistoria kwa Umoja wa Mataifa na nchi wanachama bila kusahau watetezi wa uhifadhi wa mazingira kwa kuwa mkataba wa tabianchi  utatiwa saini kwenye makao makuu ya Umoja huo New  York, Marekani. Utiaji saini huo unafanyika huku wadau wa mazingira kama vile mtandao wa usimamizi wa misitu Tanzania, MJUMITA ukiwa nao mstari wa mbele kulinda mazingira hususan maeneo ya misitu yaliyo karibu na wananchi. Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Rahima Njaidi katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii amekaribisha hatua ya utiwaji saini akisema ni jambo jema na wanalipigia chepuo kwani linaimarisha jitihada zao. Halikadhalika amezungumzia kile ambacho wanafanya na mafanikio waliyopata bila kusahau changamoto zinazowapa hamu ya kuendelea kufanya kazi hiyo kila uchao. Kwanza anaanza kwa kuelezea miradi wanayofanya.