Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO:Katika wiki ya chanjo duniani mabadiliko yawe kama ada

WHO:Katika wiki ya chanjo duniani mabadiliko yawe kama ada

Katika wiki ya kimatifa ya chanjo duniani, mwaka huu, inayoanza Aprili 24 hadi 30, shirika la afya duniani WHO linaainisha mafanikio katika chanjo, lakini pia kuorodhesha hatua zaidi zinazotakiwa kuchukuliwa na nchi kuziba pengo la chanjo na kufikia malengo ya kimataifa ya chanjo ya mwaka 2020.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Margaret Chan, mwaka jana chanjo imeleta ushindi mkubwa dhidi ya polio, surua na pepopunda kwa mama na mtoto. Lakini ushindi huo haukuwa kila mahali, polio imetokomezwa katika nchi moja, pepopunda katika mataifa matatu na surua katika ukanda mmoja.

Ameongeza kuwa changamoto hivi sasa ni kuyafanya mafanikio kuwa kama ada. Njacho inaepusha vifo milioni 2 hadi 3 kila mwaka, hata hivyo vifo milioni 1.5 vinaweza kuepukwa endapo chanjo ya kimataifa itaboreshwa.

WHO inasema leo hii watoto takribani milioni 18.7 karibu mtoto 1 kati ya 5 duniani kote bado wanakosa chanjo za kuzuia maradhi kama dondakoo, kifaduro na pepopunda.