Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania kuzungumza leo kwenye #UNGASS2016

Tanzania kuzungumza leo kwenye #UNGASS2016

Kikao maalum cha 38 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la dawa za kulevya ulimwenguni, #UNGASS2016,  kinaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo hii leo Tanzania inatarajiwa kutoa ujumbe wake. Takwimu za NACP kutoka Tanzania za mwaka 2014 zinakadiria kuwa watumiaji wa dawa za kulevya nchini humo ni kati ya 150,000 na 500,000.  Je ujumbe wa Tanzania ni nini kwenye mkutano huu? Na nini inafanya kudhibiti tatizo hilo? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.