Afrika tunayotaka inaomba utashi wa viongozi: Eliasson
Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kunafanyika kongamano Ia ngazi ya juu kuhusu ajenda ya maendeleo ya bara la Afrika, itwayo “Afrika tunayotaka”.
Lengo la mkutano huo ni kuangazia jinsi ya kuhakikisha utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Afrika ifikapo mwaka 2063, sambamba na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.
Akihutubia uzinduzi wa kongamano hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesisitiza umuhimu wa kushirikisha zaidi wanawake, kuzuia mizozo ili kukuza amani na maendeleo na hatimaye kuimarisha ufadhili wa maendeleo kupitia ushuru na usaidizi wa kimataifa. Aidha amezingatia
“Tunahitaji mshikamano, siyo tu kutoka kwa serikali, lakini pia mabunge, jamii, sekta binafsi tukitaka kutimiza malengo hayo makubwa. Malengo hayo yanahitaji hatua thabiti ili kuridhisha matarajio na matumaini yaliyoibuka duniani kote.”
(Sauti ya Bwana Kituyi)
“Nasihi sana Afrika kuangalia jinsi ya kuimarisha mikataba ya biashara huru ndani ya Afrika. Unataka biashara huru zaidi na Afrika, tayari masoko yamehurika mno (you are over liberalized) na Ulaya. Ahadi unazopewa kama motisha kwa mikataba ya biashara huru zinaondolewa kabisa wakati nchi hizi zinaingia kwenye ubia kama ule wa Transpacifik.”
Kwa upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika Erastus Mwencha akihojiwa na idhaa hii amesema tayari viongozi wameonyesha utashi wao na sasa…
(sauti ya Mwencha)