Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaosafiri kwenda Angola bila chanjo ya homa ya manjano wako hatarini kupata:WHO

Wanaosafiri kwenda Angola bila chanjo ya homa ya manjano wako hatarini kupata:WHO

Angola ambayo imekumbwa na mlipuko mkubwa wa homa ya manjano, wizara yake ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya duniani WHO na wadau wengine imepanua wigo wa kampeni ya chanjo nje ya mji mkuu Luanda ambako kumeripotiwa visa vipya. Watu milioni 2.5 wanatarajiwa kupata chanjo hiyo.

WHO pia imetoa tahadhari kwa watu wanaoishi kwenye mpaka na Angola,  lakini pia kwa wanaoingia nchini Angola bila chanjo ya homa ya manjano. Tayari visa vimeripotiwa katika nchi nyingine mbali ya Angola kama anavyofafanua Hernando Agudelo mwakilishi wa WHO Angola

(SAUTI YA HERNANDO AGUDELO)

"Wakati huu kuna visa vilivyoripotiwa DRC na vinachunguzwa, na kitu kingine watu wanaokuja hapa wakijua kwamba Angola ina mlipuko wa homa ya manjano na wanakuja bila chanjo , nchi hizo ziko hatarini kama ilivyotokea kwa Brazzaville , kwa Uchina kwa Kenya, nadhani ni wajibu wa kila mtu”