Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulaya yatangaza kutokomeza malaria, lakini bado kuna changamoto:WHO

Ulaya yatangaza kutokomeza malaria, lakini bado kuna changamoto:WHO

Ushindi mkubwa wa vita dhidi ya malaria kimataifa umetangazwa leo kwa habari njema kwamba Ulaya sasa haina tena malaria wamesema wataalamu wa afya wa Umoja wa mataifa. Flora Nducha anaarifu zaidi

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO idadi ya visa vya malaria barani Ulaya imeshuka kutoka takribani 91,000 mwaka 1995 hadi surufi mwaka jana. WHO imezitaka mamlaka za afya Ulaya kutoachana na kinga  kwa sababu kisa kimoja tu kitakachoingizwa barani humo.

Shirika hilo limepongeza ushindi huo wa vita dhidi ya malaria Ulaya kuwa ni muhimu kama sehemu ya mkakati unaoongozwa na Umoja wa mataifa wa kutokomeza malaria duniani.

Akizungumza kabla ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani itakayofanyika Jumatatu April 25, Dr Nedret Emiroglu wa WHO ameonya kwamba bara hilo litasalia kwenye hatihati hadi ugonjwa utakapotokomezwa duniani kote.

(SAUTI YA DR NEDRET)

Wakati wote kuna hatari ya kuingizwa kwa ugonjwa huo, ambayo tumeishuhudia huko nyuma, ulizuka tena na hatutaki hili kutokea. Hivyo lengo letu ni kuhakikisha tunasalia katika maambukizi sufuri na hata kuwa makini zaidi na ufuatiliaji na kuendelea kudhibiti mazalia”