Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wanapaswa kulindwa na si kampuni nyonyaji- de Zayas

Wananchi wanapaswa kulindwa na si kampuni nyonyaji- de Zayas

Mfumo uliomo kwenye mikataba ya biashara ambao unatoa fursa kwa wawekezaji na serikali kusuluhisha migogoro ya kibiashara, ISDS, unazidi kudidimiza utawala wa kisheria na demokrasia.

Hiyo ni kauli ya mtaalamu huru kuhusu uendelezaji wa mfumo wa biashara ya kimataifa wenye demokrasia na usawa, Alfred de Zayas aliyotoa leo mbele ya bunge la Baraza la haki za binadamu la Ulaya.

Amesema mifumo hiyo inaepusha kupigwa faini kwa wawekezaji wanaokiuka haki za kijamii au mazingira akitolea mfano Canada, Ujerumani, Marekani  na Colombia.

Bwana de Zayas amehoji suala la kwamba wawekezaji wanatakiwa kulindwa akisema kuwa badala yake serikali hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na wananchi wao ndio wanapaswa kulindwa dhidi ya wawekezaji wenye tamaa na kampuni nyonyaji.

Ametaka ushiriki wa kina kwa mashirika ya kiraia pindi mifumo hiyo ya usuluhishi ndani ya mikataba ya biashara inapojadiliwa ili ikuhakikisha serikali zinawajibika kulinda raia wake dhidi ya kampuni zinazolenga kuongeza faida zao huku wananchi wakiumia.