Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

O’Brien azuru Ecuador kujionea madhara ya tetemeko la ardhi

O’Brien azuru Ecuador kujionea madhara ya tetemeko la ardhi

Mratibu Mkuu wa masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Stephen O’Brien, amesafiri kwenda nchini Ecuador, kwa minajili ya kujionea mwenyewe athari za tetemeko kubwa la ardhi lililoipiga mikoa kadhaa nchini humo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akiwa Ecuador, O’Brien anatarajwa kukutana na jamii za waathirika, maafisa wa ngazi ya juu, waokozi, mashirikia ya kibinadamu, pamoja na kusaidia juhudi za kitaifa za dharura na kuchagiza usaidizi wa wadhamini katika operesheni za misaada na kujikwamua.

Kufikia sasa watu 366 wameripotiwa kufariki dunia, zaidi ya 2,600 kujeruhiwa, na wengine 231 wakiwa hawajulikani waliko.

Tayari timu ya Umoja wa Mataifa ya kutathmini na kuratibu jitihada za dharura imepelekwa Ecuador na Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), kusaidia jitihada za kitaifa.