Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwelekeo wa uchaguzi Somalia watia matumaini: Baraza la Usalama

Mwelekeo wa uchaguzi Somalia watia matumaini: Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limekuwa na mjadala maalum leo kuhusu hali ya usalama na mchakato wa uchaguzi nchini Somalia, ukihudhuriwa na Rais wa nchi hiyo Hassan Sheikh Mohamoud. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Akihutubia mjadala huo, mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Michael Keating amepongeza serikali ya Somalia na viongozi wake kwa mafanikio yaliyopatikana katika maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Miongoni mwa mafanikio hayo amesema ni kujumuisha koo na maeneo mbalimbali, kupanua idadi ya wapiga kura na kushirikisha zaidi wanawake.

Hata hivyo , amesisitiza kwamba bado hali ya usalama inatia wasiwasi, hasa kutoka kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab.

(Sauti ya Michael Keating)

“Licha ya kukabiliwa na majeruhi wengi, bado al-shabaab wanaendelea kufanya mashambulizi haramu na bila ulinganifu. Wanajaribu kuharibu mchakato wa uchaguzi ambao wanauona kama hatari kwa ajenda yao.”