Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IPU yapongeza wabunge kutendewa haki DRC na Iraq

IPU yapongeza wabunge kutendewa haki DRC na Iraq

Muungano wa mabunge duniani IPU umekaribisha mafanikio katika kesi tatu zinazohusisha unyanyasaji wa haki za bindamu kwa wabunge nchini Jmahuri ya Kidemokraia ya Congo DRC na Iraq. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA)

Katika taarifa yake IPU imesema Kamati ya haki za binadamu kwa wabunge imekuwa ikifanyia kazi kesi hizo kutafuta haki na ulinzi kwa wabunge ambapo nchini DRC , IPU imepongeza uamuzi wa mamlaka uliomuwezesha mbunge mstaafu Pierre Jacques Chalupa kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya dharura na kisha kurejea nchini.

Muungano huo wa wabunge ulikata rufaa kuhusu Chalupa kupatiwa nyaraka za kusafiri kupitia azimio lililopitishwa hivi karibuni nchini Zambia.

Katika hatua nyingine IPU imepongeza hatua ya kuachiwa huru kwa mbunge mstaafu nchini Iraq Mohamed Al-Dainy pamoja na hatua ya kuruhusiwa kutembelewa gerezani na famili yake na mwanasheria kwa mbunge Ahmed Al-Alwan.

Muungano huo wa mabunge umetaka kufutwa kwa adhabu ya kunyongwa iliyotolewa dhidi ya Ahmed Al-Alwani, kufuatia tuhuma za kuwauwa wanajeshi wawili wakati wa uvamizi nyumabani kwake mwaka 2013.