Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za misaada zinzendelea kwa Jamii zilizoathirika na tetemeko Ecuador :OCHA

Juhudi za misaada zinzendelea kwa Jamii zilizoathirika na tetemeko Ecuador :OCHA

Juhudi za misaada zinaendelea kufuatia uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi nchini Ecuador yamesema mashirika ya Umoja wa mataifa.

Tetemeko hilo la mwishoni mwa wiki lililokuwa na ukubwa wa 7.8 vipimo vya rishter ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo tangu mwaka 1979, likisabisha vifo zaidi ya 400 na maelfu kujeruhiwa.

Jens Laerke, ni msemaji wa shirika la kuratibu masula ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA...

“Uharibifu mkubwa ni katika eneo la Pedernales jimbo la Manabi ambalo serikali imelitangaza kama eneo la hatari. Fursa ya kuingia Pedernales ni finyu kutokana na kuharibika kwa miundombinu hasa barabara, kilicho bayana ni kwamba maisha ya maelfu ya watu yameathirika na tetemeko hili."

Duru zinasema tetemeko hilo pia limeathiri limebomoa majengo zaidi ya zikiwemo shule na hospital.