Skip to main content

Ban azungumza na Rais wa Sudan Kusini na makamu wa kwanza wa Rais

Ban azungumza na Rais wa Sudan Kusini na makamu wa kwanza wa Rais

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amezungumza leo na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit kwa njia ya simu. Ban amempongeza Rais huyo kwa uamuzi wake wa kumkaribisha tena Riek Machar kwenye serikali na kumuapisha kama makamu wa kwanza wa Rais Jumatatu April 18.

Ametoa wito wa kuharakisha utekelezaji wa mipango ya usalama iliyoainishwa kwenye mkataba wa amani na kuondolewa kwa vikosi zaidi vya SPLA kutoka Juba.

Katibu Mkuu pia amezungumza na makamu huyo wa kwanza wa Rais Riek Machar. Amekaribisha hatua yake ya kurejea tena Juba serikalini na kumtaka kufanya kazi kwa karibu na Rais Kiir ili kuepusha machafuko zaidi Sudan Kusini.

Ban amesisitiza umuhimu wa kuundwa haraka serikali ya mpito ya muungano wa kitaifa kama hatua muhimu kwa hatua ijayo ya mchakato wa amani katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu.