Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuyeyuka kwa barafu mlima Kenya ni athari za mabadiliko ya tabia nchi:UM

Kuyeyuka kwa barafu mlima Kenya ni athari za mabadiliko ya tabia nchi:UM

Wafanyakazi wawili wa Umoja wa mataifa wamepanda mlima Kenya wiki iliyopita kwa lengo la kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu lakini pia kutanabaisha athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha kuyeyuka kwa barafu kwenye mlima huo.

Wafanyakazi hao Newton Kanhema  na Bo Sorensen ambao pia wamepandisha kileleni bendera ya Umoja wa mataifa na ile ya malengo ya maendeleo endelevu SDG’s, wamesema wameshuhudia barafu inavyoyeyuka kwenye mlima Kenya  ambao ni chanzo kikubwa cha maji kwa taifa hilo la Afrika ya Mashariki, na kutoa wito wa hatua kuchukuliwa kunusuru vizazi vijavyo kama anavyofafanua Bernad Kiziiri kutoka ofisi ya habari ya Umoja wa mataifa Nairobi.

(SAUTI YA BERNAD KIZIIRI)