Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asihi nchi zilizoendelea kutimiza ahadi za usaidizi

Ban asihi nchi zilizoendelea kutimiza ahadi za usaidizi

Trilioni za dola zinakadiriwa kuhitajika kila mwaka kufadhili utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye mkutano wa Baraza la Kijamii na Kiuchumi unoafanyika leo mjini New York Marekani. Priscilla Lecomte na taarifa kamili.

(Taarifa ya Priscilla)

Mkutano huo unafuatilia matokeo ya kongamano la ufadhili kwa maendeleo lililofanyika mwaka uliopita mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo zaidi ya ahadi mia zilitolewa kuhusu hilo.

Ban amesema kutokana na ukuaji dhaifu wa kiuchumi na mizozo ya kimataifa, uwekezaji zaidi unahitajika kutoka kwa sekta binafsi na serikali katika kuimarisha ustawi wa jamii, akitaja miundombinu, huduma za maji safi na salama, elimu na ulinzi wa kijamii.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa nchi zilizoendelea kuongeza usaidizi kwa nchi maskini zaidi duniani, akisema

(Sauti ya Bwana Ban)

“Nasihi nchi zilizoendelea kufikia lengo tulilokubaliana la dola bilioni 100 kila mwaka ifikapo 2020 na sekta binafsi kuhakikisha mitiririko ya fedha iliyokuwa sambamba na maendeleo yanayostahili kwa mazingira na yenye utoaji gesi chafuzi mdogo.”