Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaanza kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Ecuador

UNICEF yaanza kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Ecuador

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF, limefikisha msaada wa wa dawa 20,000 za kusafisha maji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoikumba Ecuador mwishoni mwa juma.

Zaidi ya watu 240 wamekufa wengiene zaidi ya 2,500 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko hilo.

Msaada huo umeelekezwa katika eneno liitwalo Pedernales ambalo ni miongoni mwa maeneo yaliyoaathirika zaidi. UNICEF imesema itaendelea kufanya kazi na mashirika ya misaada ya kibinadamu kutoa , ulinzi, maji na huduma za kujisafi pamoja na vifaa vya elimu na mahema.

Shirika hilo limesema kwamba kipaumbele kwa sasa ni kuzuia magonjwa, kuwalinda watoto wanaoweza kutengana na familia zao, msaada wa kisaikolojia kwa watoto waliotahirika an kuwapa fursa ya kusoma.

UNICEF hata hivyo imeeleza kuwa linahitaji dola milioni moja ili kufikia mahitaji ya dharura kwa watoto walioathirika kutokana na tetemeko hilo nchini Ecuador.